welcome to s-media online service

  • Delicious
  • Facebook
  • Twitter

LATEST BONGO MOVIES

ALICE and JANEL staring Hemed!
NDOA YANGU Staring kanumba
FOUR ANGLE staring King majuto

ADVERTISEMENT


Popular Posts

PICHA ZA HABARI MPYA

BEST TZ ARTIST

ADVERTISEMENT

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKANISA YALIYOHARIBIWA KATIKA VURUGU ZA WAISLAMU MBAGALA, ATOA POLE KWA WAUMINI, AWAHAKIKISHIA MKONO WA SHERIA KUWANASA WOTE WALIOHUSIKA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia uharibifu mkubwa uliofanywa katika kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu.

HABARI ZA KIMATAIFA - Rais wa Mauritania apigwa risasia

Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, anapelekwa Ufaransa kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa alipopigwa risasi... ...

MICHEZO - Masikitiko kwa Uganda

Zambia, wakiwa ugenini Kampala, waliweza kuwafunga wenyeji wao Uganda magoli 9-8 kupitia mikwaju ya penalti, na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuutetea ubingwa wao, katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013, kufanyika nchini Afrika Kusini, mwezi Januari. Mikwaju 20 ya penalti ilihitajika kubainisha ni nani mshindi na aliyeshindwa, kufuatia Uganda kutangulia bao 1-0 katika mechi ya mjini Kampala. . ....

BURUDANI - Jela yamwita Justin Bieber

MWIMBAJI kinda, Justin Bieber, huenda akafungwa miezi sita jela iwapo atapatikana na hatia ya kumpiga Paparazi aliyetaka kumpiga picha huko Los Angeles. ...

MOVIE AND FILM - NDOA YANGU YA KANUMBA IPO MADUKANI SASA

Movie ambayo watanzaniaa wengi waliisublia kwa hamusasa yatoka ...

Afya yetu


LISHE BORA KWA WATU WENYE AFYA NZURI KWA LIKA ZOTE MTU MZIMA HADI MTOTO MCHANGA






• Kula chakula bora kunamaanisha kula vyakula aina tofauti ya vyakula kila siku kama vile matunda,
mboga, maziwa na aina ya vyakula vyenye asili ya nyama wa kufuga kama kuku, mbuzi, ngombe,
samaki na na vyakula vya nafaka.
• Lishe bora linamaanisha pia kula chakula ambacho hakina mafuta mengi, sukari au chumvi nyingi
• Zingatia angalau vyakula vya nafaka kama vile mtama, mahindi, mchele, ngano, wimbi, ndegu,
njegere. n.k
• Ni bora kula matunda mengi kama ‘maembe, ndizimbivu, papai, pera, chungwa, ubuyu, nanasi,
pesheni, zambarau” na mbogamboga kama vile “mchicha, majani ya mboga, karoti, nyanya
chungu, nyanya, mkunde, biringanya” mara tano kwa siku.
• Kama mboga na matunda hazipatikani ni bora kununua zile ambazo zimehifadhiwa tayari
kwenye mikebe au zile ziko kwenye jokofu (friji).
• Punguza kula vyakula ambavyo vinapikwa kwa mafuta mengi na chumvi nyingi
• Lishe bora hukusaidia wewe na jamii yako kuishi vyema, kuwa na afya bora, kufanya kazi vizuri na kwa bidii, shuleni na hata kucheza.
MAELEZO 2
UNYONYESHAJI BORA WA MAZIWA YA MAMA
• Maziwa ya mama pekee ndio chakula na kinywaji cha mtoto bora zaidi kwa watoto kwa miezi
sita ya kwanza.
• Ni jambo la muhimu sana kunyonyesha watoto wachanga kwa muda wa miezi minne na
uendelee kunyonyesha hadi mtoto atakapofikisha mwaka mmoja na kuendelea.
• Mtoto akifikisha miezi sita ndio wakati muafaka wa kumpa vyakula vya nyongeza vilivyotayarishwa
katika hali ya usafi.
• Onana na mnasihi akushauri kuhusu muda na jinsi ya kumuanzishia mtoto wako vyakula vya
nyongeza
• Vyakula vya ngogeza viwe ni vya mchanganyiko wa makundi yafuatayo ya chakula:- vyakula
vya nafaka, venye asili ya nyama, mbogamboga na matunda, mafuta na sukari (kiasi). Lisha kila
chakula kwa siku kadhaa kwa kufuatanisha kabla hujaaza chakula chengine kipya.
• Usimuachilie mtoto alale kama chupa ya maziwa ingali mdomoni, ili kuepukana na kuoza kwa
meno na madhara ya.
• Watoto wanaopewa maziwa ya mama pekee hawaugui mara kwa mara, na
wakiugua, makali ya ugonjwa hupungua na hupona mapema kwa sababu yale
maziwa ya mwanzo ya njano yenye viini vingi vya kumkinga dhidi ya magonjwa.
MAELEZO 3
CHAKULA BORA KWA WATOTO WENYE AFYA
• Watato nao pia wanahitaji chakula bora tu kama vile watu wazima lakini kwa vitengele ambavyo
vinaambatana kulingana na umri wao.
• Lisha watoto vyakula tofauti tofauti kila siku, pamoja na matunda, mboga maziwa na aina
yeyote ya vyakula vyenye asili ya nyama, samaki na maharagwe (nafaka).
• Punguza kiasi cha sukari kwenye vinywaji vyao na ulaji wa peremende kwa watoto.
• Punguza pia kiasi cha chakula ambacho hupikwa kwa mafuta ya kuchemka kama vile keki, viazi
karai, vitumbua, kababu, sambusa, chapatti, soseji, aiskrimu za maziwa, biskuti na vyakula vyote
vya kutumbukizwa kwenye mafuta.
• Maziwa ni muhimu sana kwa utengenezaji wa meno na mifupa ambayo yenye nguvu.
• Ulaji wa chakula bora husaidia watoto kuwa na afya bora, kuwa na nguvu, kufanya
vyema masomoni, na kupunguza uzito wa mwili usiohitajika.
MAELEZO 4
KAA MCHANGAMFU NA AFYA BORA
• Pata angalau dakika thelathini (30) ya mazoezi kila siku kwa na kama vile lisaa limoja kwa
watoto.
• Ongeza mazoezi ya mwili kwa mkataba wako wa kila siku hasa kwa kupanda gazi, kuelekeza
gari lako mbali na mahali unapotaka kwenda ile utembee mwendo kufikia mahali hapo.
• Ile hali ya kutembea ni jambo rahisi na pia sio ghali na unaweza kufanya hili tendo kuwa la kila
siku.
• Panga mazoezi ya kila siku kwa jamii yote na ufurahie mazoezi kama vile kutembea, kucheza
uwanjani, kupalilia shamba, na pia kucheza nyimbo.
• Watoto wanapaswa kucheza nje mahala kuna upepo mzuri wala sio ndani ya nyumba au
kutazama runinga (televisheni).
• Madaktari wanahimiza kuwa sio bora watoto wadogo chini ya miaka miwili kutazama televisheni
kabisa, na watoto ambao wako zaidi ya miaka miwili wanapaswa kutazama televisheni kwa
muda usiozidi masaa mawili na waangalie vipindi ambavyo vinaambatana na umri wao.
• Changamsha mazoezi ya kimwili wakati mko ndani ya nyumba kama vile michezo, kuruka
kamba, na kucheza nyimbo.
• Kuwa kwenye hali ya uchangamfu kunakusaidia wewe pamoja na jamii yako kuishi
kwa afya njema, kujisikia vizuri na kuwa na uzito wakiasi.
MAELEZO 5
WAKATI WA KULA NI WAKATI WA JAMII KUWA PAMOJA
• Tayarisha chakula bora kwa jamii yako na mle pamoja kama familia.
• Tumia huo wakati wa kula pamoja ili kujua hali ya watoto wako na vile walivyoshinda siku
nzima na pia kuzungumzia juu ya utamaduni na ubora wa mila zetu.
• Usiwaruhusu watoto kuangalia runinga(televisheni) au kucheza michezo ya kanda (video)
wakati wa kula.
• Ile hali ya kula pamoja hutia nguvu familia na kuiunganisha pamoja.
• Watoto wale ambao wanakula na familia zao kila wakati hukua vyema na pia
hufanya vizuri kwenye masomo.
• Watoto wale pia ambao hula pamoja na jamii zao huwa wana uhusiano mwema
kwenye jamii.
MAELEZO 6
DUMISHA UZITO WA KAWAIDA WENYE AFYA
• Unapaswa kufahamu ya kwamba unakula zaidi kama unazindisha kulingana na vile mwili wako
unavyohitaji.
• Unapokula zaidi na haufanyi aina yeyote ya mazoezi ya kujenga mwili, unaweza kupata uzito au
unene mwingi kupita kiasi.
• Kuishi kwa ile hali ya kuwa na uzito wa mwili vyema, ni muhimu kwako kula chakula bora na
kwa kiasi.
• Kuna njia muafaka ambazo unaweza kufanya ili kudumisha ule uzito wa mwili ambao unaofaa,
kama vile:-
- kupunguza jinsi unavyokula mafuta na sukari
- kupunguza kiasi cha chakula
- kuacha kula tu mradi umeshiba
- kuongeza kufanya mazoezi ya mwili
• Kudumisha uzito wa mwili bora unakusaidia wewe kutokana na hatari kama vile:-
- kuumwa na viungo vya mwili
- kupandwa na damu
- ugojwa wa sukari
- ugojwa wa moyo
- ugojwa wa saratani
MAELEZO 7
USAFI BORA KWA CHAKULA SAFI
• Daima nawa mikono yako kwa sabuni na maji yanayotiririka kabla ya kupika na kula chakula.
• Osha vizuri matunda na mbogamboga zinazoliwa bila kupikwa. Ili kuhifadhi vitu bichi kama vile
mboga, mboga za majani, osha kabla ya kupika.
• Weka nyama ambayo haijapikwa na vyakula aina ya samaki kando na vyakula vingine.
• Vyakula kama vile maziwa, nyama na samaki zaweza kuhifadhiwa kwa jokofu (friji).
• Baada ya kupika chakula, safisha na upanguze meza na vibao vyote vile ulivyokuwa ukivitumia
kwa maji safi na yenye sabuni.
• Usiache chakula ambacho kimepikwa juu ya meza kwa muda mrefu au zaidi ya masaa mawili
• Hifadhi makombo ( chakula kilichobakia) kwenye mikebe ambayo ina vifuniko na uweke ndani
ya jokofu (friji).
• Kudumisha usafi mwema wakati unavyotengenezea jamii yako chakula kunafanya
magojwa kukaa mbali na jamii yako.
• Kuhifadhi chakula kwa njia bora husaidia jamii yako kujikinga na magojwa kutokana
na ile hali ya chakula ambacho kimeharibika.
MAELEZO 8
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUNUNUA CHAKULA
• Panga na utayarishe orodha ya mahitaji ya chakula inayoendeshana ni kasi cha pesa kilichopo
kabla ya kuenda dukani au sokoni.
• Si vyema kwenda kununua chakula wakati wa njaa kwani mara nyingi utajikuta unanunua vyakula
ambavyo si muhimu.
• Soma maelezo (lebo) pale inapobidi kununua vyakula vilivyosindikwa kando ya mikebe ya chakula
kwa makini na uchague vyakula ambavyo havina mafuta mengi, sukari au chumvi nyingi.
• Tumia vibali kwa bidhaa unazohitaji.
• Tazamia sana kununua bidhaa ambazo ziko kwenye mauzo ya kipekee na ambazo unaweza
kuziona wakati huo huo kwenye mauzo.
• Linganisha bei ya bidhaa tofauti na ununue zile bora kwa bei ya chini ili kuokoa pesa zako.
• Kama mboga na matunda ziko kwa bei ya juu, unaweza kununua zile ambazo zimehifadhiwa
kwenye jokofu (friji) au mikebe maalum.
• Nunua tu kile ambacho ulichokiandika kwenye ile orodha yako ya ununuzi pamoja na vitu vile


ambavyo ni vya maana zaidi ndio uweze kutayarisha chakula kama vile ulivyopanga.